Monday, November 11, 2013

Messi aumia tena, safari hii ni mguu wa kushoto

Injury: Messi picked up his injury while sprinting for the ball
Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi akichezewa rafu na beki wa Real Betis katika mchezo wa jana. Rafu hii ilimfanya Messi atolewe nje katika pindi cha kwanza na nafasi yake kuchukuliwa na Iniesta. Majeraha haya yamekuwa ya pili kwa Messi msimu huu, ikiwa imepita wiki mbili tu tokea amalize matibabu ya mejeraha mengine aliyoyapata mwezi wa tisa. Mara ya kwanza aliumia kwenye goti la mguu wa kulia na mara hii ameumia kwenye kifundo cha mguu wa kushoto. Bado haijajulikana itamchukua muda gani nje ya uwanja, ripoti kamili juu yake itatolewa leo baada ya uchunguzi. Majeraha haya yatanarajiwa kuendelea kumpoteza Messi kwenye ramani ya soka msimu huu, kwani hadi sasa utegemezi wake ndani ya klabu ya Barca umepungua na pia ameshazidiwa kwa kiasi kikubwa kwa ufangaji wa magoli na wapinzani wake Ronaldo na Diego. Katika mchezo huu kati ya Barcelona na Real Betis, Barcelona ilishinda magoli 4-1, magoli ya Barcelona yalifungwa na Neymar, Pedro na Fabregas mawili. 

Injury worry: Lionel Messi picked up an injury when sprinting for the ball and had to be withdrawn
Withdrawal: But he was substituted after just 21 minutes

No comments:

Post a Comment