Kocha mpya wa Sunderland Di Canio leo amendeleza mbwembwe zake za ushangiliaji akiwa kiwanjani tofauti na makocha wengine walivyozoeleka. Picha hii inamuonesha Di Canio akiruka juu takribani mita moja na nusu baada ya filimbi ya mwisho kupigwa na Sunderland kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila dhidi ya Evarton. Mbwembwe za Di Canio zilianza wiki iliyopita baada ya kukimbia na kuteleza kwenye majani baada ya goli la pili kufungwa katika ushindi wa goli tatu kwa bila dhidi ya Newcastle. Kabla ya Di Canio, Jose Mourinho kocha wa Real Madrid ndiye aliyekuwa anaongoza kushangilia kwa mbwembwe lakini kwasasa Di Canio ni kiboko ya wote.
|
Saturday, April 20, 2013
Di Canio amendeleza mbwembwe za ushangiliaji
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment