Monday, April 22, 2013

Man utd mabingwa wa BPL 2012/13

Magoli matatu yalifungwa na Robin Van Persie leo yameiwezesha Man utd kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza mara ya ishirini 20. Man utd imetwaa ubingwa baada ya kuifunga timu ya Aston Villa magoli matatu kwa bila. RVP aliyekuwa mwiba mkali kwa Aston Villa amefunga magoli yote katika kipindi cha kwanza dakika za 2, 13 na 33. Kwa ushindi huu Man utd imefikisha pointi 84 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote. 

Bango linaloonesha namba ya RVP ikiwa inafanana na idadi ya vikombe vya BPL Man utd iliyoshinda hadi sasa



Tap in: Robin van Persie opens the scoring for Manchester United
RVP, Rafel na Carrick wakishangilia goli la kwanza alilofunga RVP katika dakika ya pili ya mchezo

Stunning double: Robin van Persie volleyed home Manchester United's second goal
RVP akijiandaa kuachia shuti kufunga goli la pili kati ya magoli matatu aliyofunga katika kipindi cha kwanza kwenye mechi ya ubingwa kati ya Man utd na Aston Villa. Goli hili ni moja kati ya magoli bora aliyowahi kufunga RVP. RVP amefunga magoli katik dk yaa 2, 13 na 33.

RVP hii ni mara yake ya kwanza kushinda kombe la ligi katika maisha yake ya soka, akielezea katika mahojiano aliyoyafanya na Skysport, RVP amesema, "leo ni siku ya historia katika maisha yangu, nimefunga magoli matatu, timu yangu imeshinda kikombe cha ligi na mimi nimepata medali ya kwanza ya kombe la ligi, nilikuwa ninahamu sana ya kushinda kombe la ligi nashukuru leo ndoto yangu imetimia, nina furaha sana' 

No comments:

Post a Comment