Hatimaye kocha wa Man city Roberto Mancini amefukuzwa kazi baada ya kushindwa kutimiza malengo ya klabu hiyo ya mwaka huu ikiwemo kutetea kombe la ligi na kufika robo fainali ya UEFA champions. Nafasi yake itashikilia kwa muda na kocha msaidizi Brian Kidd ambaye ataiongoza timu kwenye mechi mbili za ligi zilizobakia. Wakati huo huo uongozi wa Man city bado upo kwenye harakati za kumpata kocha wa Malaga Pellegrini ili aweze kuziba pengo la Mancini. |
No comments:
Post a Comment