Shabiki mmoja anayesemakana kuwa ni baba wa mchezaji wa zamani Liam Kelly amefariki dunia akiwa
kiwanjani kwa ugonjwa wa moyo. Shabiki huyo mwenye umri wa miaka 50 alikuwa uwanjani kuangalia mpambano kati ya Kilmarnockn na Hibernian
nchini Scotland. Shabiki huyo alianguka chini ndipo wenzake walipombeba na
kumuweka sehemu ya wazi ili atibiwe na madaktari wa timu, baada ya muda si
mrefu gari la wagonjwa lilifika na kumchukua lakini alifariki dunia muda
mchache baada ya kufika hospitali. Kufuatia tukio hili makocha wa timu zote
mbili walikubaliana mchezo ughairishwe hadi siku nyingine ambapo hadi tukio
linatokea matokeo yalikuwa goli 1-1.
Polisi na madaktari wa timu zote mbili wakimpatia shabiki huyo huduma ya kwanza |
Gari la huduma ya kwanza likiwa uwanjani kumbeba shabiki huyo na kupelekwa katika hospitali ya jirani na uwanja wa Rugby Park
Mashabiki wa mpira wenye magonjwa ya upumuaji ikiwemo moyo wameombwa kuwa makini kushiriki sehemu zenye msongamano mkubwa wa watu ndani ya viwanja ili kuepukana na matukio kama haya.
|
No comments:
Post a Comment