Moyes kocha mpya wa Man utd leo ameongea na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza baada ya kutangazwa kama kocha mkuu wa Man utd. Katika maongezi ya leo Moyes amesema "sikuwa na mpango wa kuhama Everton, na nilishapanga mipango ya mwaka ujayo kwa Everton lakini ofa ya Man utd ilipokuja sikuweza kukataa kwasababu ni timu kubwa, lakini kwasasa bado nipo Everton na nitahakikisha tunashinda michezo yote iliyobakia, vile vile napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru sana mashabiki wa Everton, wachezaji na uongozi mzima wa Everton, wameishi na mimi vizuri kwa kipindi chote cha miaka 11, bado nawapenda na nitaendelea kuwa nao daima na nitawasaidia kutafuta kocha mpya badala yangu. Everton kwasasa ipo nafasi ya sita ikiwa na pointi 60 na imebakiza michezo miwili dhidi ya West Ham itakayochezwa tarehe 12 na ya mwisho watacheza dhidi ya Chelsea tarehe 19.
![]() | |
|

No comments:
Post a Comment