Timu ya Bunge la jamhuri ya Muungano la Tanzania jumamosi ya wikiendi hii ilishuka tena dimbani na vikosi viwili tofauti vya mpira wa miguu kucheza na timu za Konyagi pamoja na NMB. Mechi hizi zote ilifanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, ambapo katika mchezo wa kwanza timu ya Bunge iliambulia kichapo cha magoli 3-0 dhidi ya Konyagi Tanzania, magoli yote ya Konyagi yalifungwa katika kipindi cha kwanza dakika za 10, 20 na 25. Kwa ushindi huu timu ya Konyagi Tanzania iliweza kuondoka na kombe pamoja na medali wakati timu ya Bunge wao walipata medali peke yake. Mh. Khalifa kutoka Zanzibar alipewa tuzo maalumu kwa kuiongoza vyema timu yake akiwa kama nahodha. Mechi ya pili ilikuwa ni kati ya NMB na kikosi cha pili cha timu ya Bunge kilichoongozwa na Mh Ngwali, ambapo timu ya Bunge ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya NMB Tanzania, na kwa upande wa netiboli timu ya Bunge iliweza kutoka na ushindi wa magoli 39-17 dhidi ya NMB. Mgeni rasmi katika mechi hizi alikuwa ni Mh George Mkuchika na meneja wa timu ya Bunge alikuwa Mh Kasim Majaliwa. Zifuatazo ni picha zinazoonesha matukio mbalimbali ya michezo hii
|
Kikosi cha Konyagi Tanzania- Mpira wa miguu kilichoshinda magoli 3-0 dhidi ya Bunge |
|
Kikosi cha Konyagi na Bunge kwenye picha ya pamoja |
|
Kikosi cha NMB Tanzania kilichofungwa na Bunge goli 1-0 |
|
Wachezaji wa timu ya Bunge netiboli walioshinda dhidi ya NMB magoli 39-17, hapa walikuwa wakiwashangilia wenzao wa mpira wa miguu |
|
Nahodha wa timu ya Konyagi akikabidhiwa kombe baada ya ushindi dhidi ya timu ya Bunge. Kulia mwenye jezi ya bluu ni Mh Khalifa akiwa amenyanyua juu tuzo yake aliyopewa kwa kukiongeza vyema kikosi cha Bunge |
|
Kikosi cha Bunge kilichoshinda dhidi ya NMB Tanzania |
|
Kikosi cha Bunge kilichofungwa dhidi ya Konyagi Tanzania |
No comments:
Post a Comment