Ripoti kutoka kwenye vyombo vya habari vya nchini Brazil inasema, michuano ya kombe la mabara inayoendelea nchini humo inaweza kusimama kutokana na maandamano yanayofanywa na wakazi wa jiji la Rio de Janeiro. Waandamanaji hao wanapinga kufanyika kwa michuano hii na ile ya kombe la dunia nchini Brazil wakidai kuwa inatumia gharama kubwa wakati huduma nyingi za kijamii nchini Brazil ni duni. Serikali ya Brazil kwa ujumla itatumia paundi bilioni 26 kwenye michuano yote mitatu (kombe la mabara, olimpinki na kombe la dunia) fedha ambazo wanachini wa Brazil wanasema zingetumika kwenye mambo mengine ya kimaendeleo nchini humo ili kupunguza matatizo ya wananchi. Hadi sasa watu wengi wamejeruhiwa vibaya na uharibifu mkubwa umeshafanyika kwenye mitaa mbalimbali ya jiji hilo. FIFA wenyewe wamesema wanaamini vurugu hizo zitasimama lakini vyombo vya habari vya nchini Brazil vimeripoti kuwa maandamano hayo hayatasimama hadi kombe la dunia hadi serikali ya Brazil iwapatie huduma muhimu wakazi wa Brazil. Zifuatazo ni baadhi ya picha zinazoonesha matukio mbalimbali ya vurugu hizo za waandamanaji
No comments:
Post a Comment