Klabu ya Arsenal imefikiana makubaliano ya mwanzo na klabu ya Real Madrid kumsajili mshambuliaji Gonzalo Higuain kwa paundi mil 22 na kumlipa mshahara wa paundi 150,000 kwa wiki. Mazungumzo baina ya klabu hizi mbili bado yanaendelea ila taarifa za mwanzo kama zilivyonukuliwa na gazeti la Sportsmail zinasema wakati wowote muafaka utafikiwa na Higuain atatangazwa rasmi kuhamia Arsenal. Usajili huu kwa Arsenal utavunja rekodi kwani kabla ya Higuain mchezaji ambaye alikuwa anashikilia rekodi ya kusajiliwa kwa pesa nyingi na Arsenal alikuwa ni Andrey Arshavin kwa paundi mil 15 mwaka 2009. Hatua hii ya kutaka kumsajili Higuain kwa fedha nyingi ni jitihada ambazo kocha wa Arsenal Arsene Wenger ameanza kuzifanya ili kuijenga tena Arsenal yenye ushindani na uwezo wa kutwaa vikombe. Muda wa usajili bado upo hivyo matarajio ni kwamba Wenger ataweza kuwasajili wachezaji wengine zaidi ya Higuain. Mbali ya Higuain Arsenal pia imehusishwa kutaka kumsajili Rooney, Fellaini, David Villa, Ashley Williams na Stevan Jovetic.
|
Thursday, June 20, 2013
Gonzalo Higuain kutua Arsenal wakati wowote
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment