1. Utamaduni wa kushangilia wanaoutumia wapenzi wa soka nchini Brazil. Wanatumia vivuvuzela vidogo, ukubwa wake upo kama vikombe, lakini pia wanatumia mipira iliyounganishwa na mishikio ya plastiki yenye rangi za kuvutia zikifanana na nguo zao.
Hivi ni vivuvuzela vidogo, vinatoa sauti kama vuvuzela kubwa, halafu vinasehemu ya kushikia ili kupuliza 'vipotabo'. Vuvuzela hizi ni moja wapo ya kivutio kikubwa kwenye fainali za Brazil kama ilivyokuwa Afrika ya Kusini. |
Hii ni aina ya mipira yenye mishikio ambayo wanaitumia kushangilia na wakati mwingine hutumika kupigia makofi kama wanavyoonekana washangiliaji. Inapendeza sana!!!!!!!!!! |
2. Fukwe maarufu duniani za Copacabana zenye mazingira mazuri ya kupumzikia na hali ya hewa safiiiiiii.
3. Chakula aina ya feijoada, ni chakula cha asili nchini Brazil, wageni wengi wanaofika Brazil hulishwa feijoada kama ishara ya upendo ya watu wa Brazil. Bila shaka feijoada italiwa vilivyo Juni na Julai mwakani
4. Ni sehemu ya Christ the Redeemer ambayo ni sanamu kubwa kuliko yote duniani, watu wengi hufika sehemu hii kupiga picha pamoja na kuangalia mandhari ya Brazil kutoka juu ya mlima. Christ the Redeemer ni moja ya vivutio saba vya dunia, hutembelewa na watu takribani mil 2 kwa mwaka na idadi hii ya watu inategemea kuongezeka mara mbili zaidi mwakani wakati wa kombe la dunia.
5. Utamaduni wa watu na ngoma za asili (Samba) hii ni michezo na ngoma za asili ambazo chimbuko lake ni biashara za utumwa kwenye karne ya 16 hadi 19. Utamaduni wa Samba umeenea sana duania kutokana na soka pamoja na aina ya uchezaji wa ngoma zenyewe. Wachezaji wengi wa soka kutoka Brazili wanakawaida ya kushangilia magoli kwa kucheza samba. Kutokana na umaarufu wake duniani shirika la kimatiafa la sayansi UNESCO mwaka 2005 lilitambua Samba kama moja ya utamaduni wa mwanadamu unaotakiwa kulindwa kwa karne zijazo. Watu wengi duania hupenda kwenye nchini Brazil kushudunia ngoma hizi za Samba ambazo hufanyika kwenye kiwanja kikubwa nyakati za jioni hadi usiku. Utamu wa kombe la dunia vilevile utakolea ukichanganyikana na ngoma za Samba. Hakika watakaokwenda hawataichoka Brazil.
6. Ubora wa soka la Brazil, hakuna asiyefahamu kiwango cha Brazil katika soka. Ni nchi ambayo imeshashinda kombe la dunia mara nyingi kuliko zote. Licha ya kuwa na timu dhaifu kwasasa, lakini wapenzi wengi wa soka wanaamini timu hiyo itakuwa imara zaidi pindi michuano hii itakapo anza hivyo wengi watapenda kuona kama Brazil wataweza kulibakiza kombe nyumbani mbele ya Hispania, Ujerumani, Uholanzi, Italia, Ufaransa na Argentina.
No comments:
Post a Comment