Timu za taifa za Brazil na Hispania zimefanya mazoezi ya mwisho mwisho kabla ya kukutana leo (Juni 30) kwenye mechi ya fainali itakayofanyika saa saba usiku kwa masaa ya Afrika Mashariki. Mchezo wa leo utakuwa ni wa kuvutia kwani Hispania itahitaji kuchukua kombe la tatu baada ya kushinda kombe la dunia na kombe la Ulaya. Brazil wao wametoa ahadi ya kuvunja rekodi ya Hispania ya kutofungwa tokea mwaka 2010 na vilevile wanahitaji kurudisha heshima yao, kwani Brazil kwasasa ipo nafasi ya 22 kwenye renki za FIFA jambo ambalo ni aibu kwa nchi kama Brazil. Brazil na Hispania zimeshakutana mara nane, kati ya hizo Brazil imeshinda mara nne na Hispania mara mbili na michezo miwili ilikuwa sare.
Brazil
Hispania
No comments:
Post a Comment