Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA limemchagua Bi. Lydia Nsekera kutoka Burundi kuwa mjumbe wa kamati kuu ya FIFA kwa miaka minne mfululizo. Bi. Nsekera anakuwa ni mwanamke wa kwanza kuwa mjumbe kwenye shirikisho hilo kwa kipindi kirefu jambo ambalo limetafsiriwa kuwa ni jitihada za FIFA katika kudumisha usawa wa kijinsia kati ya wakike na kiume kwenye kufanya maamuzi ndani ya shirikisho hilo ikizingatiwa kuwa mchezo wa mpira wa miguu huchezwa na jinsia zote. Mbali ya kuwa mjumbe wa kamati kuu ya FIFA Bi. Nsekera pia ni rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Burundi tokea mwaka 2004 na pia ni mjumbe wa kamati kuu ya olimpiki duniani.
No comments:
Post a Comment