Klabu ya Everton imeitolea nje Man utd kuwanunua wachezaji wake wawili Marouane Fellaini na Leighton Baines kwa paundi mil 28. Man utd walikuwa wamepeleka ofa ya kumsajili Fellaini kwa paundi mil 16 na Leighton kwa paundi mil 12, jumla ni paundi mil 28, pesa ambazo zimeonekana kuwa ni ndogo kulinganisha na thamani ya wachezaji hao. Mbali ya udogo wa ofa ya Man utd, uongozi wa klabu ya Everton kupitia kocha wake Roberto Martinez, umesema, klabu ya Everton haiwezi kumuuza Fellaini kwasababu muda wa mauzo wa mchezaji huyo umekwisha tokea Julai 31, hivyo klabu inayotaka kumnunua mchezaji huyu ingojee hadi msimu ujao. Fellaini alisajiliwa na Everton mwaka 2008 kwa paundi mil 15 akitokea Standard Liege na Leighton alisajiliwa na Everton mwaka 2007 akitokea Wigan kwa paundi mil 6.
No comments:
Post a Comment