Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA, linatarajia kufanya mkutano mkuu mwezi wa kumi mwaka huu ili kubadilisha tarehe za michuano ya kombe la dunia mwaka 2022 nchini Qatar. Taarifa kutoka Sportsmail zinasema, FIFA ina mpango wa kuifanya michuano hiyo ichezwe mwezi Disemba badala ya Juni. Kufuatia taarifa hizi vyama mbalimbali vya soka duniani ikiwemo chama cha mpira cha Uingereza, Ujerumani, Italia na Hispania vimepinga vikali uamuzi huo wa FIFA. Vyama hivyo vimepinga uamuzi wa FIFA kwasababu utaingilia michuano ya ligi za ndani na kombe la Ulaya, ambayo huwa inaanza mwezi wa nane hadi wa tano mwaka unaofuata. Vyama hivyo vimepanga kuandikia barua FIFA ili kuzuia uamuzi huo kupitishwa. FIFA imepanga kubadilisha tarehe za michuano hiyo kutoka mwezi wa Juni hadi Disemba kutokana na hali ya joto kwenye nchini ya Qatar kuanzia mwezi wa tano hadi wa nane. |
Monday, August 12, 2013
FIFA kubadilisha tarehe ya kombe la dunia oktoba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment