Rais wa Cameroon, Paul Biya amemshawishi mwanasoka Samuel
Eto'o kutafakari upya mipango yake ya kujiuzulu kutoka soka ya kimataifa.
Mshambuliaji huyo wa Chelsea alikutana na wawakilishi wa Rais mjini Yaounde
kujadili mustakabali wa mchezaji huyo kuhusu soka ya kimataifa. Baada ya maongezi, Eto'o alikubali kurudi na kuichezea Cameroon kwa mara nyingine. Hivyo anatarajiwa kwenda Ufaransa kujiunga na wenzake kujiandaa kucheza dhidi ya
Tunisia mechi ya kufuzu kombe la Dunia Brazil mwaka 2014.
Etoo
mwenye umri wa miaka 32, mapema mwaka huu aliwaambia wenzake kuwa hatacheza tena soka ya nyumbani
punde tu baada ya Cameroon kushinda dhidi Libya na kuingia katika awamu ya pili ya
kufuzu kwa kombe la dunia. Licha ya uamuzi wake wa kuacha soka la kimataifa, kocha
wa timu ya Cameroon Volker Finke alimteua Eto'o kuchezea timu ya taifa ya
Cameroon dhidi ya Tunisia ingawa mwenyewe hakuwa ametoa taarifa rasmi. Eto'o
amekuwa na uhusiano mbaya na maafisa wa soka nchini Cameroon katika siku za
nyuma ikiwemo hata kuongoza timu ya taifa kwenye mgomo uliosambaratisha mechi ya
kirafiki dhidi ya Algeria. Eto’o aliadhibiwa kwa kupigwa marufuku kucheza mechi 15
ingawa baada ya kukata rufaa alipunguziwa adhabu hadi mechi 8. Hata baada ya
adhabu yake kumalizika alikataa kuichezea Cameroon kwa miezi kadhaa. Pia sio
mara ya kwanza kwa Rais Biya kuingilia kati na kumzuia mchezaji kujiuzulu
kutoka katika majukumu ya kitaifa.
|
Thursday, October 10, 2013
Eto'o akubali ombi la Rais kurudi timu ya taifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment