Madaktari wa klabu ya Liverpool watalazimika kumfanyia uchunguzi mshambulijia wa klabu hiyo Luis Suarez baada ya kufanyiwa rafu mbaya na mchezaji wa Everton Mirallas. Rafu aliyofanyiwa Suarez ilionekana ni mbaya na ilitakiwa mchezaji huyu kutolewa nje lakini aliweza kuvumilia na kumka tena. Kocha wa Liverpool katika mahojiano baada ya mchezo alisema, alishangazwa na kitendo cha refa kutokutoa kadi nyekundu kwa mchezaji wa Everton, kutokana na rafu mbaya aliyoicheza. Pia alisema, rafu hii inaweza kuathiri kiwango cha Suarez kwenye mechi zijazo.
No comments:
Post a Comment