Done Deal: Kiungo wa Chelsea Juan Mata amesajiliwa na klabu ya Man utd kwa dau la paundi mil 37. Mata anatarajiwa kufanya vipimo kabla ya kutambulishwa rasmi kwa mashabiki wa klabu hiyo. Taarifa kutoka DailyMail zinasema kocha wa Chelsea Jose Mourinho ameshasaini makataba wa kumuuza mchezaji huyu kwenda Man utd licha ya kuwa mashabiki wa Chelsea hawajapendezwa na kuuzwa kwa mchezaji huyu. Mata anatarajia kutambulishwa wikiendi hii na ataweza kucheza mechi yake ya kwanza akiwa na United dhidi ya Cardiff City siku ya jumanne.
Tweet mbalimbali zinazoongelea uhamisho wa Mata kwenda Man utd
No comments:
Post a Comment