
Klabu ya Arsenal imeweka sanamu ya Dennis Bergkamp nje wa uwanja wake Emirates kama kumbukumbu ya mchezaji huyu nguli wa zamani. Bergkamp amepewa heshima hii kutokana na mchango wake mkubwa kwa klabu ya Arsenal kipindi akicheza tokea mwaka 1995 alipojiunga akitokea Inter Milan. Tokea ajiunge na Arsenal Bergkamp aliweza kucheza zaidi ya mechi 400, kufunga magoli 120 na kushinda makombe makubwa saba akiwa chini ya kocha Arsene Wenger. Mbali ya Bergkamp, sanamu zingine za wachezaji nguli wa Arsenal ambazo zipo nje ya uwanja wa Emirates ni Tony Adams na Thierry Henry.



Sanamu ya Bergkamp ilitokana na picha hii siku ambayo mchezaji huyu alionesha uwezo mkubwa wa kumiliki mpira kwenye mechi kati ya Arsenal na Newcastle mwaka 2003.
No comments:
Post a Comment