Friday, February 7, 2014

Wapinzani wa Azam FC watua Dar Es Salaam

Wapinzani wa Azam FC kwenye mechi za kimataifa timu ya Ferroviario wakiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dar es Salaam baada ya kuwasili jioni hii. Ferroviario itakwaana na Azam FC jumapili jioni kwenye uwanja wa Azam Complex. Ferroviario wanaingia leo na shirika la ndege la Msumbiji saa tisa kasorobo. Timu ya Azam FC yenyewe inaendelea na maandalizi kwenye kambi yake iliyopo Chamazi. Mechi itachezwa kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi jumapili saa kumi kamili jioni na kurushwa na Azam TV

No comments:

Post a Comment