Picha ya kushoto inamuonesha golikipa wa Barcelona, Victor Valdes akirukia mpira huku mguu wake wa kulia ukiwa umepinda jambo ambalo lilimfanya ategue goti lake. Picha ya kulia ni Valdes akisaidiwa na mchezaji mwenzake kuvua soksi ili kuangalia jeraha alilopata. Baada ya kutolewa uwanjani na kufanyiwa vipimo madaktari wamesema Valdes amevunjika goti na itambidi kufanyiwa upasuaji na kumfanya akae nje ya uwanja kwa miezi sita. Taarifa hizi zimekuwa ni mbaya kwa kocha wa Barcelona kwani timu yake inakabiliwa na mechi ngumu za muhimu kipindi hiki ikiwemo kombe la ligi, mfalme na Uefa champions. Lakini pia Valdes ndiye kipa tegemezi wa timu ya taifa la Spain kwa msimu huu ambao Casillas amekuwa benchi kwenye mechi za ligi. Hivyo Spain itabidi itafute mbadala wa Valdes kati ya Reina na De Gea kwa ajili ya kombe la dunia nchini Brazil.
No comments:
Post a Comment