Wednesday, April 10, 2013

Beckham amenifanya niwe huru - Ibrahimovic

Mshambuliaji wa PSG Zlatan Ibrahimovic amesema kusajiliwa David Beckham kumemfanya awe huru  na purukushani za waandishi wa habari. Ibrahimovic alisema “ tokea nimefika nchini Ufaransa watu wengi pamoja na waandishi wa habari wamekuwa wakinizonga nikiwa kama supa staa pekee, nilikuwa napata shida sana, kila ninapokwenda waandishi na watu wananizonga lakini tokea David Beckham amefika nimekuwa huru sana kwasababu umati wote wa waandishi umehamia kwake, Beckham ni supa staa kunizidi mimi, yeye anajulikana sana duniani, pia David ameshazoea kupambana na mapaparazi tofauti na mimi". Zlatan Ibrahimovic (31) alijiunga na PSG kutoka Ac Milan mwishoni mwa msimu uliyopita na David Beckham amejiunga na PSG mwanzoni mwa mwaka huu akitokea LA Galaxy ya Marekani.  

No comments:

Post a Comment