Sunday, August 25, 2013

Man utd ipo tayari kumuuza Rooney nje ya nchi

Going nowhere: Man United have ruled out selling Wayne Rooney to Chelsea
Sportsmail linaripoti kuwa klabu ya Man utd imemruhusu Rooney kuhama ila sio kwa klabu iliyopo ndani ya ligi ya England. Sportsmail limesema taarifa hizi zimetoka kwa ofisa mmoja wa United ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema, 'klabu ya Man utd ipo tayari kumuuza Rooney muda wowote ila haiwezi kumuuza kwa klabu pinzani za Arsenal au Chelsea'. Ofisa huyo aliongeza kwa kusema 'hata kama Chelsea wataongeza dau la mamilioni ya paundi, Rooney hawezi kuuzwa kwenda Chelsea'. Taarifa hizi zinazipa uhuru klabu za Real Madrid, Monaco na PSG ambazo bado hazijakamilisha zoezi la usajili. 

No comments:

Post a Comment