Kiungo wa Real Madrid, Mesut Ozil, ameonesha kuchukizwa na kitendo cha kocha wake kumtoa mapema kipindi cha pili kwenye mechi kati ya Granada na Madrid. Katika kuonesha hasira zake Ozil alikwenda moja kwa moja ndani ya chumba cha kubadilishia nguo badala ya kutaa kwenye benchi pamoja na wachezaji wenzake. Tokea Ancelotti awe kocha wa Madrid, Ozil amekuwa akianzia benchi na mara nyingi kufanyiwa mabadiliko kwenye kipindi cha pili. Uwepo wa Isco na Modric ndiyo umekuwa kikwazo kikubwa kwa Ozil kupata nafasi ya uhakika kwenye kikosi cha kwanza. Hata hivyo, Ozil alishaonesha nia ya kutaka kuhama na tetesi za mwazo zinasema wakala wa Ozil alishafanya mazungumzo ya awali na klabu ya Man utd.
Video: Angalia Ozil alivyopitiliza hadi chumba cha kubadilishia nguo kuonesha hasira zake za kutolewa kipindi cha pili
No comments:
Post a Comment