Saturday, February 22, 2014

Uwanja mbovu wa Ferroviario ndiyo sababu kubwa Azam FC kutolewa Afrika. Picha hizi zinaonesha hali halisi ya uwanja huo

Hizi ni picha zinazoonesha hali halisi ya uwanja wa Ferroviario uliyotumika kwenye mechi ya marudiano dhidi ya Azam FC nchini Msumbiji. Azam FC ilifungwa magoli 2-0 kwenye mechi hii na sababu kubwa ikiwa ni mazingira mabovu ya sehemu ya kuchezea mpira iliyokuwa imejaa matope na maji kama inavyoonekana kwenye picha. Ikumbukwe tu kuwa Azam FC ndiyo klabu yenye uwanja wenye pichi nzuri ya kuchezea kuliko klabu yoyote nchini Tanzania jambo ambalo limewafanya wachezaji wake kuzoea kucheza katika mazingira mazuri kuliko waliyokutana nayo nchini Msumbiji. 




Fananisha na Azam Complex 

No comments:

Post a Comment