Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers amekubali matokeo baada ya kukiri kuwa klabu yake haiwezi kuwa bingwa wa ligi mwaka huu. Akiongea na Sportsmail Rodgers alisema 'Kwa sisi kama Liverpool bado kufukiria ubingwa. Nilikwenda kwenye mechi ya juzi kati ya Man city na Chelsea nikaangalia kwa makini vikosi vya timu zote mbili (Man city na Chelsea), nikagundua kuwa wenzetu wana vikosi madhubuti sana, sisi kama Liverpool kushindana nao kwasasa ni vigumu mno. Liverpool bado tunajenga timu, itachukua muda kufikia hatua waliyonayo wenzetu, kwani na wao walianza kama sisi. Ila kwavile tupo kwenye mashindano kama timu lazima tuseme tunashindania ubingwa, lakini kusema ukweli bado ni mapema sana kwa Liverpool kufikia hatua ya kuchukua ubingwa'. Hayo ni maneno ya Rodgers akiongelea hali halisi ya klabu yake. Msingi wa maneno ya Rodgers ni kuwa Liverpool bado ipo kwenye hatua ya kujenga timu na lengo kuu la timu msimu huu ni kuingia nne bora ili kupata nafasi ya kushiriki kombe la mabingwa Ulaya (Uefa). Hadi sasa Liverpool inashikilia nafasi ya nne ikiwa na pointi 47 na imezidiwa pointi nane na vinara Arsenal wakati Chelsea na Man city wapo nafasi ya pili na tatu wakiwa na pointi 53.
No comments:
Post a Comment