Klabu ya Barcelona imesema itamfanyia uchunguzi mshambuaji wake Lionel Messi baada ya kutapika uwanjani wiki hii. Taarifa hizi zimetolewa na kocha wa Barca, Tata Martino alipokuwa kiongea na waandishi wa habari akisema ' bado hatujafahamu tatizo ni nini, lakini madaktari walipomfanyia vipimo vya awali wamesema sio tatizo kubwa. Uchunguzi zaidi utaendelea kufanyika juu ya afya yake'. Messi alitapika uwanjani kwenye mechi ya kirafiki kati ya Argentina na Romania. Hii ni mara ya pili mchezaji huyu kutapika uwanjani baada ya ile mechi kati ya Bolivia na Argentina ambapo Messi alishindwa kucheza na kutapika kutokana na hali ya hewa ya Bolivia iliyopo ukanda wa juu wenye hewa kavu.
No comments:
Post a Comment