Mshambuliaji tegemezi wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar ameumia jana jioni akiwa mazoezini pamoja na wachezaji wenzake. Neymar ameumia kwenye kifundo cha mguu wake wa kulia baada ya kuteguka wakati akitaka kumkaba Willian. Baada ya kuumia madaktari wa timu walimfanyia uchunguzi na kugundua kuwa Neymar hakupata majeraha makubwa ndipo walipompa mapumziko kidogo kabla ya kuendelea na mazoezi. Neymar anatarajiwa kuendelea kufanya mazoezi na wenzake huku akifanyiwa uchunguzi zaidi na mategemeo kuwa maendeleo yake yatakuwa mazuri hivyo kumuwezesha kucheza kwenye mechi ya ufunguzi siku ya Alhamisi dhidi ya Croatia.
No comments:
Post a Comment