Kiungo wa Barcelona, Xavi yupo mbioni kujiunga na klabu ya Qatar, Al Arabi. Taarifa hizi zimetolewa na gazeti la Marca likisema, wakala wa Xavi, Rais wa Barcelona pamoja na viongozi wa klabu ya Al Arabi walifanya kikao na kukubaliana kwa kusaini mkataba wa awali. Rais wa Barca Josep Maria amesema atamruhusu Xavi kuondoka Barca kama mchezaji huyo atakubali mwenyewe kuondoka. Xavi aliyelelewa na klabu ya Barca tokea utoto wake, anaweza kuondoka Barca msimu huu baada ya kujihisi kushuka kiwango jambo ambalo linamfanya aondoke Barca kabla ya kuuzwa kwa lazima au kusugua benchi.
No comments:
Post a Comment