Kocha mkuu wa timu ya Simba, Patrick Liewig alimwaga machozi
kwenye hotel waliyofikia jijini Mwanza baada ya mchezo kati ya Toto na Simba
kuisha. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya goli mbili kwa mbili.
Kocha huyo alisema inamuuma sana kuona Simba inatoka droo kwenye mchezo ambao
walikuwa na uwezo wa kushinda. Kocha Liewig alisema ulikuwa ni uzembe tu wa
mabeki, wachezaji hawachezi kwa moyo mmoja, itabidi tukae pamoja wachezaji na
uongozi ili tuweze kujadili hali hii ya Simba, matatizo mengi ya timu yanaanzia
kwenye uongozi sio wachezaji pekee (hisani ya gazeti la mwananchi)
No comments:
Post a Comment