Video inaonyesha siku Ronaldinho alipopigiwa makofi na washabiki wa Real Madrid kama ishara ya kumkubali kwa kiwango alichoonesha kwenye mechi kati ya Real Madrid na Barcelona mwaka 2005. Katika mechi hiyo iliyofanyika tarehe 19 mwezi wa 11, Barcelona ilishinda goli 3 na chachu ya ushindi huo ulitokana na kiwango cha juu alichoonesha Ronaldinho. Tukio hili la kihistoria ni nadra sana kutokea hususani barani ulaya kwa mashabiki kupiga makofi kwa timu pinzani tena kwenye uwanja wa nyumbani. Tujikumbushie kwa kucheki video.
No comments:
Post a Comment