Mnamo Januari mwaka huu, Sepp Blatter, raisi wa FIFA alipendekeza uwezekano wa kuanzishwa vikwazo na sheria zitakazo vibana vilabu ambavyo mashabiki wake watahusika na ubaguzi wa rangi, ikiwemo kushushwa daraja na kupokonywa pointi, lakini sasa anaonekana kuulegeza msimamo huo kwa kusema sheria hiyo itasababisha mashabiki kujaribu makusudi kushinikiza mechi kusitishwa na hali hiyo italeta tabu zaidi na kufanya mchezo wa soka kupoteza utamu ila alisema ni lazima kitu kifanywe kuhusiana na suala hilo, hususani mwezi Mei kwenye mkutano wa baraza kuu la FIFA ambapo swali la ubaguzi litakuwemo kwenye ajenda. Ubaguzi wa rangi imekuwa tatizo kubwa katika mchezo wa soka jambo ambalo lisiposhughulikiwa mapema litaufanya mchezo huo kupoteza hadhi yake. Tunaamini Blatter ataweza kulisimamia na kuleta sheria zitakazo komesha kirusi hichi cha ubaguzi katika soka.
No comments:
Post a Comment