Zulu Mramba (Mipango) |
Mashindano ya kikapu Taifa yamezidi kupamba moto jijini Tanga, ambapo jana Timu ya chuo cha Mipango Dodoma kilipata ushindi mtamu kwa kuwalambisha Tanga United vikapu 80 - 78 katika mchezo uliofanyika jana tarehe 4 April. Jana pia kulikuwa na mchezo mwingine kati ya Vijana na Bandari Tanga, katika mchezo huu mwamuzi alijikuta akisimamisha mchezo baada ya umeme kukatika, lakini baada ya dk 30 umeme ulirudi na hadi mwisho wa mchezo Vijana waliweza kuibuka washindi kwa vikapu 63 - 56.
No comments:
Post a Comment