Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) imezipongeza timu za Ashanti United ya Dar es Salaam, Mbeya City ya Mbeya
na Rhino Rangers ya Tabora kwa kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao
(2013/20114). Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wallace Karia amezitaka timu hizo
kufanya maandalizi ya kutosha ili ziweze kushindana katika VPL ikiwemo kutimiza
masharti ya kuwa klabu za Ligi Kuu. Moja ya masharti ya klabu zenye hadhi
ya Ligi Kuu ni kuwa na timu ya pili (U20) ambayo itakuwa na inacheza mechi za
utangulizi kwenye uwanja wa nyumbani kila timu ya wakubwa inapocheza. Mbali
ya kuthibitisha timu hizo tatu kupanda daraja, pia Kamati ya Ligi imethibitisha
rasmi timu tatu zilizoshuka daraja kurudi Ligi ya Mkoa katika mkoa husika. Timu
zilizoshuka kutoka Daraja la Kwanza (FDL) ni Small Kids ya Rukwa kutoka kundi
A. Kundi B timu iliyoshuka ni Moro United ya Dar es Salaam wakati Morani
FC ya Manyara yenyewe imeporomoka kutoka kundi C.
No comments:
Post a Comment