Mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho kati ya Azam na AS FAR Rabat ya Morocco iliyochezwa juzi (Aprili 20 mwaka huu) imeingiza sh. 50,850,000. Fedha hizo katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa timu hizo kutoka suluhu zimetokana na watazamaji 8,268 waliokata tiketi. Viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 10,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000 ambacho kilikuwa kiingilio cha juu kwa jukwaa la VIP A. Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 7,354. Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; gharama za tiketi sh. 5,575,500, asilimia 15 ya uwanja sh. 6,791,175, asilimia 10 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 4,527,450 na asilimia 75 iliyokwenda kwa klabu ya Azam ni sh. 33,955,875. Vilevile, Mechi iliyopita ya Azam katika michuano hiyo dhidi ya Barrack Young Controllers II ya Liberia iliingiza sh. 44,229,000 kutokana na watazamaji 17,128 waliokata tiketi.
No comments:
Post a Comment