Klabu ya Tottenham inataka kuweka rekodi ya dunia ya uhamisho
wa mchezaji wake tegemezi Gareth Bale baada kutanganza bei ya mchezaji huyo
ambayo ni paundi milioni 100. Mwenyekiti wa Tottenham Levy alisema klabu yake
inachohitaji ni hizo pesa tu ili kumwachia Bale kuondoka Tottenham, kauli
ambayo wengi wameitafsiri kama tishio ili vilabu vinavyomuhitaji vikate tamaa.
Hadi sasa uhamisho wa Cristiano Ronaldo wa paundi milioni 80 kutoka Man utd
kwenda Real Madrid ndiyo unashikilia rekodi ya dunia, lakini, kama Tottenham
watafanikiwa kuumuza Bale kwa paundi milioni 100 uhamisho huo utazidi ule wa
Cristiano Ronaldo na Bale ndiye atashikilia rekodi ya dunia. Klabu ambazo
zimeshatangaza kumhitaji Bale ni pamoja na PSG, Real Madrid na Bayern Munich.
Klabu hizi tatu zinazomuhitaji Bale zinauwezo wa kulipa paundi mil 100, ila kubaki
au kuondoka kwa Bale kutategemea matokeo ya mwisho ya ligi kuu nchini
Uingereza, kwani uongozi wa Tottenham umesema hautakuwa tayari kumuuza Bale
kama Tottenham itapata nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa ulaya (UEFA
champions) msimu ujao.
No comments:
Post a Comment