Dempsey (Tottenham) akishangilia baada ya kufunga goli la kwanza kati ya magoli matatu yaliyofungwa dakika 15 za mwisho yaliyoifanya
Tottenham kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Man City. Matokeo haya
yanaifanya Tottenham irudishe matumaini yake ya kuwania nafasi ya nne kwenye
msimamo wa ligi wakiwa kwenye ushindani mkali dhidi Chelsea na Arsenal. Tottenham
bado wapo nafasi ya tano wakiwa na pointi 61 wakati Chelsea wanaocheza na
Liverpool leo wapo nafasi ya nne na pointi 61 na Arsenal nafasi ya tatu
pointi 63. Chelsea itahitajika kushinda mchezo wa leo ili kujiweka katika nafasi nzuri
ya kushiriki UEFA msimu ujao. |
Sunday, April 21, 2013
Tottenham 3 - 1 Man City
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment