Klabu ya Arsenal inatarajia kulipwa paundi mil 3 na
Barcelona mwishoni mwa msimu huu ikiwa ni moja ya makubaliano kwenye mkataba wa
kumsajili Fabregas na Alex Song. Barcelona iliwasajili Fabregas na Song mwaka
2011 na 2012 na moja ya makubaliano kwenye mkataba huo ni kwamba ,kama
Barcelona itafanikiwa kushinda ubingwa wa ligi italipa paundi mil 3 kwa Arsenal
ikiwa ni sehemu ya faida iliyopata kutokana na wachezaji hao. Cesc Fabregas
alisajiliwa na Barcelona akitokea Arsenal kwa paundi mil 35 na makubaliano
yalikuwa kwamba, Cesc atailipa Arsenal paundi laki 8.8 kila mwaka kwa miaka
mitano kutoka kwenye mshahara wake na vilevile Barcelona itailipa Arsenal paundi
mil 4.4 kama Barcelona itashinda makombe mawili ya ligi na moja la UEFA
champions kwa kipindi cha miaka mitano. Cesc alifanya uamuzi huo wa kulipa
mwenyewe sehemu ya ada ya uhamisho kutokana na mapenzi yake ya kutaka kurudi
nyumbani licha ya kuwa hadi sasa bado anangojea Xavi astaafu ili aweze kupata
namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Barcelona.
No comments:
Post a Comment