David Beckham amekuwa Muingereza wa kwanza kushinda makombe ya ligi mara nne kwenye nchi tofauti baada ya jana PSG kutwaa ubingwa wa ligi ya Ufaransa. Kabla ya kutwaa ubingwa na PSG Beckham ameshatwaa ubingwa na klabu za Marekani (Galaxy), Uingereza (Man utd) na Hispania (Real Madrid). Beckham (38) tokea ajiunge na PSG ameshacheza mechi 10 za ligi na mkataba wake utakwisha mwisho wa msimu huu na PSG wameshatangaza nia ya kumuongezea mkataba. PSG wametangazwa washindi wa ligi jana usiku baada ya kuwafunga Lyon kwa goli moja kwa bila, goli lililofungwa dakika ya 53 na Menez.
|
David Beckham akishangilia ushindi na Ibrahimovic baada ya mechi kati ya PSG na Lyon kuisha kwa PSG kushinda goli 1-0. Kwa matokeo haya PSG imefikisha pointi 77 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwenye ligi ya Ufaransa hivyo kutangazwa kuwa mabingwa wa 2012/13. |
Monday, May 13, 2013
Beckham Muingereza wa kwanza kushinda kombe la ligi mara nne kwenye nchi tofauti
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment