CECAFA Kagame cup ni michuano inayozikutanisha klabu bingwa za Afrika mashariki na kati ili kupata klabu bingwa katika kadi hii ya Afrika mashariki. Michuano hii inatarajiwa kuanza tarehe 18 Juni na kutoka Tanzania bara wawakilishi watakuwa wawili Yanga na Simba. Kutokana na hali hii watu wengi wamekuwa wakihoji kwanini Azam imeachwa katika michuano hiyo na katika kulijibu hilo klabu ya Azam ilitoa taarifa ifuatayo "Hata sisi kama Azam FC tungependa kushiriki lakini kuna vigezo vya kushiriki ambavyo tunadhani hatuna, awali tulidhani kwa kuwa sisi ni washindi wa pili kwenye ligi kuu kwa mwaka wa pili mfululizo na Yanga ni bingwa mtetezi na bingwa wa Tanzania basi tungeshiriki pamoja kwenye Kagame ya mwaka huu lakini kwa maelezo tuliyopata ni kuwa CECAFA na TFF wamechukua bingwa wa mwaka jana (ambaye ni Simba) na bingwa mtetezi wa Kagame Cup (ambaye ni Yanga), kwa sababu hiyo ndiyo maana sisi kama Azam Fc hatujashiriki kwenye michuano hiyo, hivyo tumeamua wachezaji wetu waende likizo na watarejea kujiandaa na ligi kuu msimu wa 2013/14.
No comments:
Post a Comment