Goli la mwaka 2002 alilofunga Zinedine Zidane kwenye fainali ya Uefa Champions kati ya Real Madrid na Bayern Leverkusen bado linashikilia rekodi ya goli bora lililowahi kufungwa kwenye fainali za michuano hiyo. Magoli mengi yameshawahi kufungwa kwenye fainali za Uefa lakini goli la Zidane bado ndiyo goli bora kuliko yote. Gazeti la Sportmail katika tafiti zake limesema goli hilo bado limebakia kuwa bora kuliko yote kutokana na mazingira lilivyofungwa kwani mpira aliopewa Zidane ulitokea juu sana na haukuwa kwenye mazingira mazuri ya kuweza kuupiga na kufunga, lakini Zinedine alitumia ujuzi wake wa hali ya juu kuweza kuupiga mpira huo na kuingia nyavuni. Zidane mwenye alishawahi kuhojiwa na kukiri kuwa kati ya magoli yote goli hili ndilo bora kuliko yote. Angalia tena ustadi wa Zidane alivyoweza kufunga goli hilo kwenye video hapo chini
No comments:
Post a Comment