Kocha wa Bayern Munich Jupp Heynckes amesema leo ndiyo itakuwa nafasi yake ya mwisho kushinda kombe la Uefa kwani muda wake wa kuifundisha timu hiyo umefikia kikomo. Heynckes aliyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mechi ya finali kati ya Bayern na Dortmund. Heynckes alisema “hii ni mara yangu ya mwisho kushinda kombe hili, nakumbuka jumamosi iliyopita ilikuwa ndiyo mara yangu ya mwisho kuingoza Munich kwenye ligi, na jumamosi hii itakuwa ndiyo mara yangu ya mwisho kuingoza timu kwenye fainali za kombe la Uefa, naamini timu yangu itaweza kuifanya siku yangu iwe ya furaha, mawazo yangu ni chanya wakati wote, niliwaza hivyo kabla ya kucheza na Juve na Barcelona na tulifanikiwa hivyo sina wasiwasi, naamini timu yangu itashinda kwani nina wachezaji wenye uwezo mkubwa”. Heynckes anatarajiwa kuachia madaraka yake ya kuifundisha Munich baada tu ya mechi hii ya fainali kwa aliyekuwa kocha wa Barcelona Pep Guardiola hivyo ni wakati mzuri kwake kuondoka Bayern Munich na historia nzuri itakayomfanya akumbukwe daima.
No comments:
Post a Comment