Katibu mkuu wa chama cha soka Afrika ya Mashariki (CECAFA) Nicholas
Musonye amevihakikishia vilabu vyote vya soka Afrika mashariki kuwa michuano ya
mwaka huu ya CECAFA Kagame Club Cup itakayofanyika nchini Sudan itakuwa salama. Michuano hiyo mwaka huu itakafanyika Sudan katika miji ya kaskazini Darfur na Kadguli kusini mwa Kordofan kuanzia tarehe 18 mwezi wa sita hadi
tarehe 2 mwezi wa saba mwaka huu. Musonye aliyasema hayo baada ya kukutana na
mkuu wa mkoa wa Darfur bwana Osmar Mohamed ambaye amehakikisha uwepo wa ulinzi
mkali katika michuano hiyo ndani na nje ya viwanja hivyo mashabiki wajitokeze
kwa wingi katika michuano hiyo. Michuano ya Kagame Cup hujumuisha klabu bingwa
zote za Afrika mashariki na kati ambapo Tanzania itawakilishwa na Yanga kutoka
Tanzania bara na KMKM kutoka Tanzania visiwani (Zanzibar).
Musonye (katibu mkuu CECAFA) wa pili kulia akiwa na Mkuu wa Mkoa Darfur wa tatu kutoka kulia wakikagua moja kati ya viwanja vitakavyotumika kwenye michuano hiyo. |
No comments:
Post a Comment