Beki wa Man city Kolo Toure amesajiliwa na Liverpool bila
ada yoyote baada ya mkataba wake na Man city kuisha. Toure anatarajiwa kujiunga
rasmi na Liverpool tarehe 1 Juni na atakuwa ni raia wa kwanza kutoka Ivory Coast
kuichezea Liverpool. Liverpool imefikia uamuzi wa kumsajili Toure ili kuziba
pengo lililoachwa na Jamie Carragher aliyestaafu mwisho mwa msimu huu. Toure
mwenye miaka 32 amecheza mechi 13 tu msimu huu akiwa na Man city na vilevile
aliachwa kwenye kikosi kilichoshiriki michuano ya Uefa champions kutokana na
upinzani mkali uliopo ndani ya klabu ya Man city kutoka kwa Kompany, Nastasic
na Lescott hivyo imekuwa ni rahisi kwa Toure kufanya uamuzi wa kujiunga na
Liverpool ili aweze kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza.
No comments:
Post a Comment