Nchini Burundi, Kilabu ya Lydia Liduc Academi, imefuzu kwa raundi ya mchujo wa kuwania kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kuishinda timu kongwe ya Asec Mimosa d' Abidjan ya Cote d Ivoire katika raundi ya pili ya fainali za kombe hilo.Lydia Lidic imekuwa ni timu ya kwanza kutoka Burundi kufikia hatua hiyo kwa zaidi ya miaka 22. Na ni timu pekee ya Afrika ya Mashariki na Kati iliosalia kwenye mashindano hayo ikumbukwe Afrika Mashariki na kati inajumuisha nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Sudan, Somalia, Eritrea na Djibouti. Hii inaonesha kwa kiasi gani nchi za ukanda huu zipo nyuma kwa maendeleo ya soka barani Afrika na dunia kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment