Nchi ya Qatar imeendelea kusisitiza kuwa inaweza kuandaa Kombe la Dunia mwaka wa 2022 katika majira ya joto (yani miezi ya tano, sita na saba) hata kama FIFA ikiendelea kushinikizwa kuhamisha michuano hiyo hadi msimu wa baridi. Taifa hilo lenye utajiri wa nishati, ambako nyuzi joto hufikia sentigredi 45 ilipewa kibali cha kuandaa Kombe la Dunia katika mazingira ya utatanishi kutokana na ukweli kwamba nchini ya Qatar haikuwa na vigezo kulinganisha na nchi zingine kama USA, UK na Australia. Qatar inasema inaweza kukubali kuhamisha hiyo hadi msimu wa baridi, lakini ikasisitiza kuwa bado michuano hii inaweza kufanyika mwezi wa tano hadi wa saba kwa kujenga viwanja vyenye hewa ya baridi na kutumia teknolojia mpya inayojali mazingira (yani viwanja vyenye air condition)
Mfano wa uwanja utakaojengwa Qatar ambao utakuwa na viyoyozi vya kupooza joto |
Njia ya kuweka viyoyozi ndani ya viwanja itatatua tatizo la joto kwa mashabiki wakiwa ndani, lakini namna ambavyo mashabiki wataweza kukabiliana na joto nje ya viwanja bado ni suala linalotia wasiwasi.
Rais wa FIFA Sepp Blatter katika kuliongelea suala hili alisema lilikuwa kosa kupanga kinyang'anyiro hicho kwenye msimu wa joto, katika taifa la jangwa. Kwa upande wa UEFA, Rais wa Shirikisho hilo, Michel Platini amesema kuwa wanachama wote 54 wa UEFA wamekubaliana kwa kauli moja kuhamisha michuano hiyo hadi msimu mwingine wa mwaka. Lakini kamati ya mandalizi ya Qatar imejaribu kuondoa wasiwasi huo, kwa kusema teknolojia ya kuleta hewa ya baridi, kwa kutumia solar, katika maeneo ya umma, nje na ndani ya viwanja, huenda ikatatua shida hizo bila shaka tutasubiri kuona jinsi namna suala hilo litakavyokwenda, nasi tutakufahamisha
No comments:
Post a Comment