Klabu ya Manchester United leo wamekabidhiwa kombe la
ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza katika mechi yao ya 35 dhidi ya Swansea
mechi iliyokwisha kwa Man utd kushinda goli 2-1. Mechi ya leo ilikuwa na mvuto
mkubwa kwa mashabiki wa soka duniani ikiwa maalumu kumuaga Sir Alex Ferguson
aliyeingoza Man utd kwa kipindi cha miaka 27. Vilevile, Paul Scholes aliyejiunga
kwa mara ya pili na Man utd mwaka 2011 naye pia leo ameagwa na washabiki wa Man utd ikiwa ni
mechi yake ya mwisho kucheza kwenye dimba la Old Trafford. Mechi ya leo pia
imetengeneza historia kwa Robin Van Persie mchezaji aliyesajiliwa kutoka
Arsenal msimu huu na leo amefanikiwa kushinda kombe la ligi kwa mara ya kwanza
katika historia ya maisha yake ya soka. Naye, Rio Ferdinand katika mechi ya leo
aliweza kufunga goli la ushindi, goli ambalo amelifunga baada ya kukaa miaka mitano bila goli. Katika
hotuba yake baada ya mechi, Sir Alex Ferguson amewatakia mafanikio mema
wachezaji wote wa Man utd pamoja na kuwashukuru washabiki wote wa Man utd kwa
kumpa “support” kipindi chote alichoitumikia klabu na kuwaahidi kuwa ataendelea
kuwa nao daima. Kwaheri Sir Alex Ferguson!!!!
|
Sir Alex ndiye aliyenyanyua kombe la ubingwa ikiwa ni ishara ya shukrani kwa mafanikio aliyoyafanikisha ndani ya klabu
|
Robin Van Persie (kushoto) akinyanyua kombe la ligi kwa mara ya kwanza katika maisha yake
Kocha David Moyes na Sir Alex wakiwaaga washibiki wa timu zao baada ya mechi
|
Rio akiachia shuti la nguvu kuandika goli la pili |
|
Rio akishangilia goli la ushindi, likiwa ni goli lake la kwanza baada ya miaka mitano |
|
Paul Scholes akiwaaga mashabiki wa Man utd waliojitokeza Old Trafford |
No comments:
Post a Comment