Katika kuifanya klabu ya Simba ijiendeshe kisasa ziadi klabu ya Simba imeingia mkataba na chuo kikuu huria cha Tanzania (OUT) ili kupata misaada ya kitaalamu katika uendeshaji wa klabu. Dhumuni la mkataba huo ni kuiwezesha klabu ya Simba kupata ushauri wa kitaalamu katika kufanikisha malengo yake ya ujenzi wa uwanja wa klabu, kuandaa academi, kujenga miundombinu ya klabu na kuimarisha vitega uchumi vya klabu hiyo ikiwemo kuuza bidhaa zenye nembo ya klabu ya Simba. Akiongea na Mwananchi, katibu mkuu wa klabu ya Simba bwana Evodious Mtawala amekiri kuhusu jambo hili na amesema mpango huu utaanza mara moja, na jopo la kiufundi kuhusiana miradi hiyo kutoka OUT lipo tayari kuanza kazi. Hatua hii ya Simba imekuja katika wakati muafaka kwani vilabu vingi barani Afrika vimeshaanza kujiendesha kibiashara na kuacha kutegemea kwa kiasi kikubwa mapato ya uwanjani. Simba ikiwa ni klabu kongwe nchini, ina washabiki wengi jambo ambalo litafanikisha malengo ya klabu hiyo kufanya biashara kwani wateja wa mwanzo wa bidhaa za Simba watakuwa ni washabiki wa klabu hiyo waliopo ndani na nje ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment