Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa Ibrahim Twaha "Messi" wa Coastal union ya Tanga. Mchezaji huyo anayesemekana kuwa alikuwa hana mkataba rasmi na Coastal amesajiliwa na Simba kwa kiasi cha shilingi milioni 30. Uongozi wa klabu ya Simba ukiongozwa na mwenyekiti wa kamati ya usajili Zacharia Hans walikutana na wazazi wa Ibra na kuwapatia kiasi cha shilingi mil 30 ndipo walipokubali kumwachia mtoto wao kuijiunga na Simba. Kuthibitisha hilo Ibra mwenyewe amekiri kuwa ameshasajiliwa na Simba na atajiunga nao msimu ujao wa ligi. Kuhusiana na usajili huu, uchambuzi umeonesha Simba wamewapiga bao Yanga ambao pia walikuwa wanamuwinda Ibra tokea mwanzoni mwa msimu huu na habari hizi zitawashitua viongozi wa kamati ya usajili wa Yanga kwani walikuwa wamejipanga kumsajili mchezaji huyo kwa msimu ujao wa ligi. Ibrahim Twaha "Messi" ni mshambuliaji tegemezi wa Coastal union ambaye alipewa jina la Messi kufuatia aina yake ya uchezaji ikifananishwa na mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi hivyo usajili huu kwa Simba ni wa maana kwani wataweza kuimarisha safu yao ya ushambuliaji ambayo ilikuwa dhaifu msimu huu.
No comments:
Post a Comment