Kocha msaidizi wa Yanga, Felix Minziro amesema kiungo wa Kinyarwanda Haruna Niyonzima ndiye mchezaji bora wa klabu hiyo kwa mwaka huu.Minziro amesema benchi la ufundi likiongozwa na kocha mkuu wa Yanga Brandts limekuwa likifanya tathimini ya wachezaji wote kipindi chote cha ligi na matokeo ya tathimini hiyo yameonesha kuwa Haruna Niyonzima ndiye bora kuliko wengine baada ya kuwabwaga wenzake wawili waliokuwa kwenye kinyang'anyiro hicho ambao ni Kelvin Yondani na golikipa Ally Mustapha. Minziro amesema Niyonzima ndiye amekuwa chachu ya ushindi wa klabu ya Yanga na anategemewa kuonesha uwezo wake katika mechi ya Yanga dhidi ya wapinzani wao wa jadi Simba itakayofanyika Mei 18. Wakati huo huo Niyonzima amekaririwa akisema mkataba wake na klabu ya Yanga unakwisha mwishoni mwa msimu huu na bado hajaongea na viongozi wa Yanga kuhusiana na kusaini mkataba upya hivyo yupo huru kuhamia klabu yoyote ikiwemo watani wa jadi Simba.
No comments:
Post a Comment