Michuano ya kuwania kombe la Ulaya chini ya miaka 21 inakwisha leo kwa hatua ya makundi huku timu ya taifa ya Uingereza ikiondoka na aibu ya kufungwa mechi zote tatu ikiwa ya mwisho bila pointi. Mashabiki wa timu hiyo waimeiponda timu hiyo kwa matokeo mabaya licha ya kupangwa kundi dhaifu. Michuano hii yenye makundi mawili, kundi 'A' ndiyo jepesi ukilinganisha na kundi 'B' lenye timu zote ngumu. Timu ya Uingereza ilimaliza mechi yake ya mwisho jana usiku kwa kufungwa goli 1-0 dhidi ya Israel. Mechi za mwisho kundi B zitachezwa leo ambapo Uholanzi watakutana na Hispania wakati Ujerumani watacheza na Urusi.
Group A(Host country: Israel)
Teams | P | W | D | L | F | A | +/- | Pts |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Italy | 3 | 2 | 1 | 0 | 6 | 1 | 5 | 7 |
Norway | 3 | 1 | 2 | 0 | 6 | 4 | 2 | 5 |
Israel | 3 | 1 | 1 | 1 | 3 | 6 | -3 | 4 |
England | 3 | 0 | 0 | 3 | 1 | 5 | -4 | 0 |
Group B(Host country: Israel)
Teams | P | W | D | L | F | A | +/- | Pts |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Netherlands | 2 | 2 | 0 | 0 | 8 | 3 | 5 | 6 |
Spain | 2 | 2 | 0 | 0 | 2 | 0 | 2 | 6 |
Germany | 2 | 0 | 0 | 2 | 2 | 4 | -2 | 0 |
Russia | 2 | 0 | 0 | 2 | 1 | 6 | -5 | 0 |
Wachezaji wa timu ya Uingereza wakitafakari baada ya kufungwa na Israel |
No comments:
Post a Comment